Klabu ya
Simba FC imelazimishwa sare ya goli 2-2 na klabu ya Mbao FC kwenye
mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara mzunguuko wa nne.
Magoli ya Simba yamefungwa na Shiza
Kichuya dakika ya 16′ na Kotei dakika 49′ huku magoli ya Mbao FC
yakifungwa na Habib Kayombo 47′ na Boniface Maganga 81′ yote
yakifungwa kipindi cha pili.
Mchezo huo ambao umechezwa kwenye
dimba la CCM Kirumba ulikuwa wenye upinzani wa hali ya juu baada ya
Mbao FC kubadili mfumo wa ushambuliaji na kufanikiwa kupata magoli
mawili.
Kwa sasa Simba wamebakia nafasi ile
ile ya pili wakiwa na pointi 8 kwenye msimamo wa VPL huku klabu ya
Mtibwa Sugar ikiongoza ligi kwa alama 9.
No comments:
Post a Comment