• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Thursday, 4 May 2017

    Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tamisemi na naibu wake wajibu maswali ya wabunge na kutoa fafanuzi kadhaa yanayohusu wizara yao

    Naibu Waziri wa nch ofisi ya Rais Tamisemi,amejibu maswali kadhaa ya msingi yaliyohusu wizara yake, na ameeleza kuwa watumishi ambao hawajalipwa stahiki zao wameendelea kulipwa na bado zoezi la uhakiki linaendelea juu ya watumishi wanaohamishwa kwenye maeneo yake.

    Lakini pia mh Rais wa wa jamhuri ya muungano wa tanzania ameahidi kulipa malimbikizo ya watumishi wa umma,na hizi ajira mpya zimelenga kupunguza uhaba wa watumishi kwenye maeneo mengi tofauti.

    Pia Waziri wa nchi ofisi ya rais tamisemi ametoa ufafanuzi juu ya udhibiti wa migogoro inayoibuka,maeneo tofauti kwenye vijiji juu ya mipaka ya maeneo hayo,hivyo serikali kwa kupitia waziri wa tamisemi amesema viongozi wa maeneo ambayo migogoro imetokea watoe taarifa rasmi kwa kufuata taratibu za kawaida ambazo zipo na zimekuwa zikitumika.

    Kumekuwa na vitendo vya kihalifu kibiti,hivyo serikali inawasaidiaje katika kuweka hali ya usalama inakaa sawa ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za uzalishaji zitakazosaidia kukua kwa uchumi wao,lakini pia kwakuwa maeneo haya yameendelea kuwekewa macho zaidi ili kuzibiti ukuaji wa mji,huu na mingine hapa Tanzania.

    Haya wameyaeleza kati ya mengi yaliyohitaji ufafanuzi baada ya maswali mbalimbali toka kwa wabunge ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.



    No comments:

    Post a Comment