Hatimae
ule mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa,unaozikutanisha Timu
ya Everton toka uingereza na timu ya Gor mahia toka nchini kenya
umeendelea leo,pale uwanja wa taifa wa Tanzania mchezo ulioletwa kwa
udhamini wa Sportpesa.
Historia
kubwa imeandikwa kwa vijana wa Gor mahia kuonesha kandanda safi
ambapo panapo dakika ya 34 ya mchezo,Rooney aliiandikia Everton goli
la kwanza ambapo dakika 3 baadae kwenye dakika ya 37 mchezaji wa Gor
Mahia “Tuyisenge”alisawazisha goli hilo ambapo matokeo yalidumu
hivyo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Hakika
mashabiki wamekutana na burudani ya hali ya juu sana,huku kipindi cha
pili kikianza kwa Gor Mahia kuweka ulinzi wa kutosha lakini kwenye
dakika ya 81 “Kieran Dowell” aliiandikia Everton goli la pili na
kufanya mchezo kumalizika kwa ushindi huo wa goli 2-1.
Tukio
moja la shabiki wa Manchester United ambaye alikuwa anashuhudia
mchezo huu alishindwa kuzuia hisia zake mpaka akaingia katikati ya
uwanja na kwenda kumkumbatia Wyne Rooney,mpaka polisi waliokuwepo
uwanjani hapo walipokwenda kumtoa.
No comments:
Post a Comment