Kampuni ya uchimbaji madini ya
Acacia imekubali kuilipa serikali ya Tanzania nyongeza ya mrabaa wa
kati ya asilimia 4 mpaka 6 kama ilivyoainishwa kwenye muswada wa
sheria mpya ya madini nchini humo.
Serikali ya Tanzania na kampuni ya
Acacia ziliingia katika mgogoro mapema mwezi tatu mwaka huu kutokana
na kuzuiliwa kwa makontena 256 ya Mchanga wa dhahabu (makinikia)
kwenye bandari ya dar es salaam baada ya kubainika kuwa Acacia haitoi
taarifa sahihi ya kiwango cha madini kilichopo katika mchanga huo
hivyo kulipa tozo zisizo sahihi kwa karibu miongo miwili.
Licha ya
kukubali kulipa ongezeko hilo Acacia imesema bado inaendelea
kutathimini athari zozote zinazoweza kujitokeza kutokana na kuundwa
kwa sheria hiyo mpya.
No comments:
Post a Comment