Nyota wa klabu ya Everton FC, Wayne
Rooney ameanza mazoezi na timu yake huku akiwa na shauku kubwa ya
kutua Tanzania kwaajili ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia
utakaopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Julai 13
mwaka huu chini ya udhamini wa Kampuni ya kubashiri michezo ya
SportPesa.
Everton inatarajia kutua Tanzania
kukipiga dhidi ya Wakenya hao katika kukamilisha michuano ya
SportPesa Super Cup ambayo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es
salaam iliyoshirikisha timu kadhaa.
Rooney ambaye ndie mfungaji wa muda
wote ndani ya klabu ya United baada ya kuichezea michezo 559 na
kufunga mabao 253 na kurudi Everton tangu anodeke miaka 13 iliyopita
amesisitiza kuwa miongoni mwa wachezaji watakao kuja nchini, kuanza
mazoezi ya pamoja na wenzake, amesema kuwa atakuwemo kwenye msafara
huo chini ya Kocha Ronald Koeman.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
31 alijiunga na Toffee alipokuwa na umri wa miaka 9 pekee ndani ya
viunga hivyo vya Goodison kisha kujiunga na United mwaka 2004 na
kuwasaidia kutwaa mataji ya Champions League, Europa League, mataji
Nagano ya Premier League , mojo la FA Cup, matatu ya League Cups na
moja la FIFA Club World Cup.
No comments:
Post a Comment