Nyota wa soka wa England Wayne
Rooney, ambaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Manchester United na
kurejea Everton amesema anasubiri kwa hamu sana safari ya kwenda
Tanzania.
"Naisubiri kwa hamu safari ya
kwenda Tanzania,naamini itakuwa nzuri sana na natumai kwamba nitaweza
kuingia uwanjani na kucheza,Huwa vyema sana unaposafiri na timu.kuwa
hotelini na wachezaji, kujumuika nao na kuwafahamu zaidi.Sijawahi
kwenda Tanzania, na kwa hivyo nasubiri sana kwenda huko".
Rooney, anayeongoza kwa ufungaji
mabao England alitia saini mkataba wa miaka miwili Goodison Park
Jumapili.Everton watacheza dhidi ya mshindi wa Kombe la Super Cup la
SportPesa, Gor Mahia kutoka Kenya, katika mechi ya kirafiki
Alhamisi.Mechi hiyo itakuwa ya kusherehekea udhamini mkubwa
uliotolewa na Sportpesa kwa Everton.
Rooney, 31, tayari anafahamiana na
baadhi ya wachezaji wa sasa wa Everton.Amewahi kucheza pamoja na
Morgan Schneiderlin, Michael Keane, Phil Jagielka, Leighton Baines na
Ross Barkley baadhi ya klabu na wengine timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment