Rais
mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa alitembelea na kuzindua
nyumba 10 za wahudumu wa afya katika kijiji cha Mkungo, Wilaya ya
Chato, Geita zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.
Akihutubia
katika uzinduzi huo Rais Magufuli aliipongeza Taasisi ya Mkapa
akisema anazipenda Taasisi zinazofanya kazi ya kuonekana na sio
zinazoongea ongea.
“Mimi
nazipenda sana Taasisi zinazofanya kazi kama hii ya Mkapa Foundation
sio zinazotaka watoto wazae wakiwa shule. Taasisi za kila siku kwenye
majukwaa mzinyime fedha, nataka Taasisi zinazofanya kazi inayoonekana
sio za kuongea ongea tu”.
“Hata
mimi yupo mtoto wa mdogo wangu amezalia nyumbani, mtoto anamuita
John, wa pili anamuita Samia lakini hakubakwa. Tunafanya ukaguzi nchi
nzima kuwajua waliotumia vibaya fedha za pembejeo ambazo ni zaidi ya
Shilingi bilioni 1.5.” Aliongeza Rais Magufuli.
Rais
Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa akimkabidhi Hati za Umiliki
wa nyumba 50 za Watumishi wa Afya kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika uwanja wa
michezo wa Mazaina Chato mkoani Geita.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa mara
baada ya kukabidhi nyumba hizo 50 zitakazotumika katika Sekta ya
Afya katika mikoa ya Kagera, Simiyu na Geita.
No comments:
Post a Comment