Jumamosi hii rapper Joseph Haule
maarufu kama Professor Jay amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku
nyingi Grace Mgonja, katika kanisa la Mtakatifu Joseph lililopo
maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam.
Sherehe ya ndoa hiyo imefanyika
katika ukumbi wa Mlimani City, ambapo watu kibao maarufu walihudhuria
pamoja na viongozi wa serikali, wabunge kutoka vyama mbalimbali hapa
nchini, wasanii na wanasiasa. Miongoni mwa watu waliohudhuria sherehe
hiyo ni pamoja na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mwenyekiti
wa chadema, Freeman Mbowe, Godbless Lema, Diamond, AY, Harmonize, na
wengine.
Wakati huo huo Kubwa zaidi
lililoonekana kufurahiwa wageni waliohudhuria katika sherehe hiyo ni
show kali iliyofanywa na AY pamoja na Diamond.Pia Diamond aliweza kumpatia bwana
harusi “Professa Jay” zawadi za kushtukiza za bidhaa zake
yakiwemo maboksi matano ya Diamond Karanga, na Manukato ya Chibu
Perfume.
No comments:
Post a Comment