President mstaafu wa awamu ya tatu
Benjamin William Mkapa amewasili kwenye Wilaya ya Chato Geita akiwa
ameambatana na mke wake Mama Anna Mkapa na kupokelewa na mwenyeji
Rais John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli.
Mzee Mkapa Jumatatu ya Julai 10
anatarajiwa kukabidhi nyumba kumi kwa hospitali ya Wilaya ya Chato
zilizojengwa kwa ufadhili wa Mkapa Foundation.
Kwenye huo msafara, mstaafu Mkapa
ameambatana na Balozi wa Japan hapa Tanzania Masaharn Yoshida ambaye
Jumatatu hiyohiyo ya July 10,2017 atakabidhi mashine ya kukamulia
mafuta ya alizeti kwa chama cha ushirika wa kilimo na masoko Chato - AMCOSS
Rais Mstaafu Benjamini William
Mkapa anatarajiwa pia kuhudhuria mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na
Mwenyeji wake Dkt John Pombe Magufuli siku hiyohiyo ya Jumatatu Julai
10,2017 kwenye uwanja wa Mazaina Chato mjini.
No comments:
Post a Comment