Baada ya
kupoteza mchezo wake wa nusu fainali dhidi ya Timu ya taifa ya Zambia
,Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars,imeshuka dimbani kuchuana na
Timu ya Lesotho kumsaka mshindi wa tatu.
Kwenye
michuano ya Cosafa inayoelekea ukingoni kwa mchezo uliofanyika pale
kwenye uwanja wa Moruleng.
Mchuano
huo ulianza huku kila timu ikikamia ili kujiweka vizuri kimatokeo na
kuufanya mchezo kuonekana mgumu kwani mpaka kipindi cha kwanza
kinamalizika hakuna timu iliyochungulia nyavu za mwenzake.lakini pia
kipindi cha pili kilionekana kuwa kigumu pia na kuufanya mchezo
kumalizika kwa suluhu kwenye dakika 90 za mchezo.
No comments:
Post a Comment