Msanii
wa muziki wa kizazi kipya “Ben Pol” amesema amefurahishwa sana na
kurejea kwa mwanamuziki wa mziki wa asili Saida Karoli kwani bado ana
uwezo mkubwa wa kuimba.amesema hayo wakati wa tamasha maalumu
lililoandaliwa kwa ajili ya kurejea kwa mwanamuziki huyo aliyetamba
zamani na nyimbo zenye asili ya kihaya ikiwa ni miaka 15 toka aanze
muziki.
Tamasha
la Rise and Fall ya Saida Karoli iliyofanyika jana usiku kwenye fukwe
za EScape One na lilikutanisha wasanii mbalimbali na viongozi
waliojitokeza kumuunga mkono mwanamama huyo ambaye alipotea kimuziki
kwa kipindi kirefu.
Amesema
kuwa, Saida bado ana uwezo mkubwa sana wa kimuziki na hilo
amelithibisha pale alipotoa wimbo wake mpya na watanzania kuukabali
kwa asilimia zote na ameendelea kuonyesha uwezo wake katika
kuimba.
Saida ametoa wimbo wake mpya ujulikanao kama Urugambo
ulio katika mahadhi ya kihaya na umeonekana kushika kasi sana, Ben
Pol aliambatana na msanii wa vichekesho anayejulikana kama Ebitokea
ambapo kwa sasa wanahisiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi.
No comments:
Post a Comment