Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma Shafi
Mpenda, amekifungia kituo cha kitengo cha utafiti wa sayansi ya tiba
asili na tiba mbadala kinachojishughulisha na kupima afya za binadamu
na kutibu magonjwa mbalimbali cha The King Solomon of Sanitarium
clinik hadi hapo wataalam wa afya watakapojiridhisha uhalali wake.
Mbali na
kukifungia kituo hicho,Mpenda amesema atawachukulia hatua kali baadhi
ya wataalam wake wa idara ya afya walioshiriki kutoa vibali feki
vilivyohalalisha kituo hicho kufanya kazi ambayo imeonekana kama
kuwatapeli wananchi.
Kwa mujibu wa Mpenda ni kwamba, kituo
hicho kupitia kwa mmiliki wake Selemani Nzaganya kimekuwa kikifanya
shughuli zake kinyume na taratibu ambapo hata leseni kutoka kwa
baraza la tiba asili kimekwisha muda wake tangu tarehe 1 januari
mwaka huu,hata hivyo bado akifanya shughuli zake bila kupata leseni
mpya jambo ambalo ni kosa kinyume cha sheria.
Alisema,
amelazimika kufunga kituo hicho kwa ajili ya kuokoa maisha ya
wansanchi kwani hata mtu aliyekutwa akihudumia wananchi hana taaluma
yoyote inayomwezesha kuhudumia wagonjwa jambo linaloonekana ni hatari
kwa afya za watu.Kwa mujibu wa Mpenda hii ni mara ya pili kufunga
kituo kama hicho na ni kampeni ya kudumu kwa wale wote wanaofanya
shughuli za kuwatapeli wananchi wa Madaba ambapo ametoa onyo kwa watu
wengine wenye tama ya kupata fedha kwa njia ya ujanja ujanja kutafuta
maeneo mengine ya kufanya shughuli zao.
Hata
hivyo kwa mujibu wa majirani ambao hawakutaka kutaja majina
yao,wameipongeza serikali kwa uamuzi wa kukifungia kituo hicho kwani
wamiliki wake walikuwa wakiwaibia wananchi.Walisema, kituo hicho
kimekuwa sehemu ya tatizo kwa sababu hata wananchi wanaohitajika
kupata ushauri na matibabu hospitalini wamekuwa wakifika katika kituo
hicho kwa kuamini kwamba watapata suluhu ya matatizo yao kumbe
wanazidisha ukubwa wa matizo waliyonayo.
Kwa upande wake mtu
aliyekutwa akitoa huduma katika kituo hicho Ezakiel Mwakatumbula
alisema, wamekuwa wanatoa huduma za matibabu kwa wa magonjwa
mbalimbali hasa magonjwa sugu kwa kutumkia dawa za mimea,chakula na
matunda.Hata hivyo alikanusha kufanya shughuli zao kitapeli na
kusisitiza kuwa huduma wanazotoa zimekuwa zikiwasaidia sana wananchi
kuokoa maisha yao.
No comments:
Post a Comment