Mshindi
wa SportPesa Super Cup 2017, Gor Mahia kutoka nchini Kenya imewasili
nchini Tanzania leo julai 11 2017, kwaajili ya mchezo wao wa
kirafiki dhidi ya klabu ya Everton kutoka nchini Uingereza.
Mchezo huyo utachezwa Alhamisi hii
Julai 13 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,Gor Mahia
wanatarajia kuanza mazoezi ya mwisho pale uwanja wa taifa jijini
Dares salaam.Huku timu ya Everton ikitarajiwa kuwasili nchini
Jumatano hii huku ikiwa na mchezaji wake mpya, Wayne Rooney
waliomsajili kutoka Manchester United.Na viingilio vya mchezo huo ni
TSh 8000/= kwa VIP C na TSh 3000/= kwa viti vya mzunguko,pia mchezo
unatarajiwa kuanza majira ya saa 11 jioni.
Tayari homa ya mpambano huo
miongoni mwa mashabiki nchini imeendelea kuwa kubwa huku wengi wakiwa
na shauku ya kuwaona nyota mbalimbali wa Everton kama vile Jordan
Pickford, Ross Barkley, Idrissa Gana Gueye na wengine wengi.
No comments:
Post a Comment