Singida
United imemaliza usajili kwa na sasa ipo tayari kwa Ligi kuu
Tanzania Bara. Singida United ambayo inatarajia kushiriki ligi kuu
kwa mara ya kwanza imefanikiwa kumchukua nahodha wa timu ya APR ya
Rwanda, Michel Rusheshangoga na beki wa kulia wa timu ya taifa ya
nchi hiyo.
Michael Rusheshangonga ambaye
ametwaa tuzo ya goli bora la msimu kwa ligi kuu ya Rwanda ametua
nchini na kwenda moja kwa moja kuungana na wenzake waliopo kambini
Mwanza.
Timu hiyo imejipanga kuleta ushindani na ikiwezekana
kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu ujao, imemtambulisha rasmi mfungaji
bora wa misimu miwili mfululizo ya ligi ya Rwanda, Dany Usengimana.
No comments:
Post a Comment