Wachezaji wa klabu ya Everton
kutoka England wamewasili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa
ziara yao ya kwanza kabisa Afrika Mashariki.Wachezaji hao na
wakufunzi pamoja na maafisa wengine wa timu walifika uwanja wa ndege
saa mbili asubuhi kutoka Liverpool.
Miongoni mwa wachezaji waliosafiri
Tanzania ni Wayne Rooney ambaye amerejea katika klabu hiyo bila
kulipiwa ada yoyote baada ya kukaa miaka 13 klabu ya Manchester
United.Mashabiki wengi wa soka ya England wamesafiri Tanzania
kushuhudia Everton wakichuana na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia katika
uwanja wa taifa wa michezo jijini Dar es Salaam.
Uwanja huo una uwezo wa kubeba
mashabiki 60,000.Rooney anatarajiwa kucheza katika mechi hiyo ya
Alhamisi.Wengi wa mashabiki waliofika nje ya hoteli wanamokaa Everton
jijini Dar es Salaam waliimba "Rooney Rooney" mchezaji huyo
aliposhuka kutoka kwenye basi kuingia hotelini.
Kulikuwa pia na kundi la raia wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao walijawa na furaha kumuona
mwenzao Yannick Bolasie.Waliimba nyimbo za kitamaduni za DR Congo
naye Bolasie akawajibu kwa kucheza.
Wachezaji hao baadaye wameelekea
shule ya watoto wenye ulemavu ya Uhuru Mchanganyiko jijini Dar es
Salaam.Shule hiyo hupokea ufadhili kutoka kwa shirika la kutoa msaada
nchi za nje la Uingereza, DFID,pia wachezaji hao wamecheza na watoto
wa shule hiyo.
No comments:
Post a Comment