Leo
tarehe 13/07/2017 majira ya jioni tutawashuhudia Everton live jijini
Dar es salaam wakichuana mshindi wa SportPesa Super Cup 2017, Gor
Mahia ya nchini Kenya.
Mchezo
huo unatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa kutokana wachezaji machachari
wa klabu hiyo akiwemo Rooney,ambaye kaonekana akipasha kabla ya
mechi yao hiyo ya kirafiki.
Everton
ambao wamefikia Hotel ya sea Cliff wameonekana kufurahia mazoezi
pamoja na mazingira ambayo wamekutana nayo pamoja na hali ya
hewa,lakini pia wamepata fursa ya kujifunza vitu mbalimbali kupitia
kwa wenyeji wao.
Baadhi
yao wamesema ni nadra wawapo ugenini kuweza kuchangamana na watu
mtaani,kwani mara nyingi wamekuwa wakibaki sehemu wanazofikia na
kuelekea moja kwa moja kwenye eneo la uwanja ambapo mechi husika
inapofanyika.
No comments:
Post a Comment