Timu ya Soka ya Everton inayoshiriki ligi kuu nchini Uiungereza
baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini
Tanzania,wameendelea kuonesha kufurahishwa na ukarimu walioupata toka
kwa Watanzania kwa kupata mapokezi yasiyo na kifani.
Kupitia akaunti yake ya mtandao wa tweeter, Rooney aliwashukuru
mashabiki wa Tanzania kwa kuiunga mkono Everton katika mchezo wao wa
kirafiki dhidi ya timu ya Gor Mahia kutoka Kenya.”Great start to
the pre-season,Special thanks to the fans supporting us in Tanzania”.
Kwa upande wa Kocha wa timu hiyo, Ronald Koeman alielezea
kufarahia ziara ya kuja Tanzania na zaidi ni kutokana na hali ya
urafiki iliyooneshwa na washabiki wa soka nchini.
Wachezaji hao wa Everton akiwemo “Rooney,Morgan Schneiderlin,
Jonjoe Kenny na Kevin Mirallas” walipata fursa ya kujifunza
tamaduni za kimsai, kujifunza kupika chakula cha asili,kutembelea
shule yenye wanafunzi wenye mahutaji maalum na pia kufanya mazoezi na
timu ya vijana wenye ulemavu wa ngozi "Albino United".
Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Mgeni
Rasmi, Marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wengine
wengi waliweza kushuhudia mchezo huo.
No comments:
Post a Comment