Mambo yamekua magumu kwa "Taifa Stars" kwani imeshindwa kupata
ushindi kwenye mechi yake ya kwanza ya kufuzu fainali za Afrika kwa
wachezaji wa ndani (CHAN) itakayofanyika Kenya mwaka 2018.Stars
ilitanguliwa kufungwa goli la mapema dakika ya 17 kipindi cha kwanza
na Dominique Nshuti.
Himid Mao Mkami akaisawazishia
Stars kwa mkwaju wa penati kunako dakika ya 34, kufuatia beki wa
Rwanda kuushika mpira kwenye penati box wakati akiwa kwenye harakati
za kuokoa hatari golini kwao.
Kocha wa Stars Salum Mayanga
alilazimika kufanya mabadiliko kadhaa baada ya beki wake wa kulia
Shomari Kapombe kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia,hivyo
“Boniface Maganga” aliingia kuchukua nafasi ya Kapombe.
Aidha pia kocha Mayanga
alimpumzisha John Bocco na nafasi yake ikachukuliwa na Stamili
Mbonde.Baada ya matokeo haya Stars inatarajia kurudiana tena na
Rwanda Julai 23, 2017 katika mchezo ambao utaamua ni timu gani
itasonga mbele hatua inayofuata.
No comments:
Post a Comment