Baada ya kummwagia fedha walipokuwa
New York bado Mayweather kaendeleza jeuri ya fedha kwa McGregor walipokutana tena
SSE Arena, Wembley, London mara hii akimtambia kwa kumuonesha saa
yenye thamani ya dollar 1.4 milioni (£1.06m), ambazo ni zaidi ya
Tsh. 3 bilioni.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Conor
McGregor kumwambia Mayweather kuwa amevaa high heels walipokuwa
kwenye ziara London kuelekea pambano lao.
Tunahesabu siku 40 kuanzia leo ili
kuifikia August 26 tarehe ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa
mchezo wa ngumi duniani kote kushuhudia pambano kati ya Floyd
Mayweather vs Conor McGregor litakalopigwa T Mobile Arena, Las
Vegas ambapo Mayweather atavuna paundi 78m sawa na Tsh. 228.3 Bilioni.
No comments:
Post a Comment