Mashindano ya Sports Extra Ndondo Cup 2017 yameendelea kwa hatua ya 16 bora, ambapo tae 16 julai kwenye uwanja wa
Kinesi walikutana “Burudani FC vs Goms United”.Huku Goms United
ikifakiwa kuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali ya Ndondo
Cup 2017 baada ya kuifunga Burudani FC kwa bao 1-0.
Kocha wa Goms United Shabani
Kazumba ‘Mourinho’ amesema alishaawambia watu tangu jana mechi
yao ya leo angeimaliza ndani ya dakika 90 kama ilivyokuwa.
“Niliwaambia watu tangu jana
nitamaliza mechi ndani ya dakika 90 namshukuru Mungu ametusaidia
imekuwa hivyo. Maagizo niliyowapa wachezaji wameyatekeleza na ndio
kimetupa ushindi”, Shabani Kazumba
Kwa upande wa kocha wa Burudani
Sultani Kipuga yeye amesema bahati ilikuwa kwa wapinzani wao kwa
sababu vijana wake wamecheza vizuri.”Sultani Kipuga wenzetu
walituzidi bahati lakini uwezo tunafanana kabisa”,Sultani Kipuga.
No comments:
Post a Comment