Mchezaji
namba tano kwa ubora wa mchezo tenesi Roger Federer ameweka historia
ya kuwa mchezaji wa kwanza kutwaa taji la michuano ya Wimbledon, kwa
mara nane.
Federer
ametwaa taji hilo la Grand Slam baada ya kumshinda mpinzani wake
Marin Cilic, kwa jumla ya seti tatu.Katika
seti ya kwanza bingwa huyu wa kihistoria alishinda kwa 6-3, kisha
akashinda kwa 6-1 na kumaliza kwa 6-4, katika mchezo ulichezwa kwa
muda wa saa moja na na dakika 41.
Hili
ni taji la 19 la Grand Slam, kwa mchezaji huyu raia wa Switzerland,
na kuwa mchezaji mkubwa zaidi kutwaa mataji yote ya michuano ya wazi
ya England
No comments:
Post a Comment