Leo Julai 17, 2017 Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu imeombwa kuahirisha kesi ya utakatishaji fedha
inayowakabili Rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake kutokana na
upelelezi kutokamilika.
Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU,
Leonard Swai ameomba Mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili
ya kutajwa kutokana na upelelezi kutokamilika ambapo Hakimu Mkazi
Mkuu,Wilbard Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 31, 2017.
Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu
Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa Shirikisho hilo,
Nsiande Mwanga walifikishwa Mahakamani leo wakikabiliwa na mashitaka
28, ikiwemo ya utakatishaji fedha Dola za Marekani, 375,418.
Aidha, Jamal Malinzi na wenzake,
wamepata Mawakili wapya watatu Richard Rweyongeza, Nehemia Nkoko na Abraham Senguji kwa ajili ya kuwawakilisha katika kesi
hiyo ambao walitambulishwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.
No comments:
Post a Comment