Leo ni Siku kubwa kwa
mchezo wa mpira wa miguu nchini hususan washabiki na mchezo huo
murua, baada ya kamati ya nidhamu kuitengua adhabu yangu ya kufungiwa
mwaka mmoja,kujihusisha na masuala ya kandanda ndani na nje ya nchi.
“Adhabu hii ilikuwa
inaiumiza sana klabu yangu na kuiondolea haki yake muhimu, ya kuwapa
habari kwa wakati watanzania juu ya kinachoendelea kwenye
klabu”.
“Kiukweli niishukuru kamati ya nidhamu chini ya
Mwenyekiti wake Tarimba Abbas kwa kuiondoa adhabu hii, kiukweli
alioondolewa adhabu sio Haji, ni Simba na mchezo wenyewe wa
Soka”.
“Hakika hawa wamesikia kilio cha wengi, na kilio
cha wengi kina nguvu ya Mungu Mwenyezi, Shukran kwa Mola kwa kuwapa
nguvu hii kina Tarimba na wenzake.Niwashukuru pia viongozi wa TFF kwa
utashi wao kwenye hili”.
“Nitakuwa mjinga nisipowashukuru
wanasimba wenzangu ambao siku zote wamekuwa upande wangu, hawa
ninawaahid kuwatumikia kwa moyo na dhamira ileile ya Haji ya
kuhakikisha haki na wajibu wetu kama klabu unatekelezwa”.
“Kipekee
niwashukuru viongozi wangu wa Simba ambao walihakikisha jambo hili
linapatiwa ufumbuzi wa haraka na linamalizika kwa njia ya
amani.niwashukuru watu wote mliokuwa nami ktk sala na dua
zenu,hususan kwenye kipindi kigumu cha adhabu.Sitapenda kufukua
makaburi, yatupasa sote tusonge mbele, hakuna aliyeshinda, umeshinda
mchezo wa soka”.
Nawaahidi kuendelea
kufanya kazi zangu kwa weledi,nidhamu na kwa kuzingatia miiko ya
mchezo huu unaobeba dhamana za maisha ya watu walio wengi, sambamba
na kuendelea kuitetea na kuilinda klabu yangu kwa nguvu
zote-amesisitiza Manara
No comments:
Post a Comment