Rais mstaafu wa awamu
ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria
kwenye msiba Linah George Mwakyembe, ambaye ni mke wa Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe.
Wengine waliofika
kumfariji na kutoa salamu zao za pole Dkt Mwakyembe , Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi, Mbunge wa Chalinze Ridhiwani
Kikwete,Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyarandu, Mbunge wa
Sengerema, William Ngeleja,Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda,
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji, Waziri wa Ulinzi,
Dk Hussein Mwinyi, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga na
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Benard Membe, Waziri
Mstaafu wa Mambo ya Nje.
Kifo cha Mke wa Dkt
Mwakyembe kilitokea Jumamosi katika hospitali ya Agha khan alipokuwa
akipatiwa matibabu.
Mwimbaji wa Bongofleva
Diamond Platnumz, Mameneja wake Said Fella na Babu Tale,Lava lava ni
miongoni mwa mastaa wa Bongo waliofika nyumbani kwa Waziri wa Habari
Dr. Mwakyembe kutoa pole kufuatia kifo cha Mke wake Linah George.
No comments:
Post a Comment