Wamiliki wa vituo vyote vya mafuta
nchini Tanzania wamepewa siku 14 kufunga na kuanza kutumia mashine za
kielektroniki za kutolea risiti la sivyo wafutiwe leseni.
Rais Magufuli, ambaye ametoa agizo
hilo, ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji kuhakikisha vituo vyote vya mafuta nchini
vinatumia mashine hizo ambazo kwa Kiingereza zinafahamika kama
Electronic Fiscal Petrol Printer na kusisitiza kuwa wamiliki
watakaokiuka agizo hilo vituo vyao vifungwe na kufutiwa leseni.
"Na kwa hili natoa siku 14,
wale wenye vituo vya mafuta wote, uwe upo Chato, uwe Biharamulo, uwe
Kagera, uwe Dar es Salaam hakikisha una hiyo mashine, ndani ya siku
14," amesema Dkt Magufuli
.
Mwishoni mwa wiki Mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA) ilivifungia vituo vya mafuta kutokana kutotimiza
vigezo baada ya kutofunga mashine za kielektroniki kwenye pampu za
mafuta.Mamlaka ya mapato ilisema wamiliki wa vituo hivyo wamekuwa
wakikwepa kulipa kodi kwa kutofunga mashine hizo.
Wakati wa kuanza kutekelezwa kwa
agizo hilo Jumapili, vituo 710 vilifungiwa nchi nzima lakini baadaye
vituo 469 vikafunguliwa baada ya kulipia mashine hizo kwa mawakala
watano walioidhinishwa kufunga mashine hizo kwa vituo vyote takribani
1800 kwa nchi nzima.
No comments:
Post a Comment