Timu ya taifa ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 ya Tanzania "serengeti boys",imepata upinzani mkali toka kwa vijana wa cameroon
ambapo wamecheza mchezo wa marudiano wa kujipima nguvu.
Mchezo ambao umekuwa mgumu kwa upande wa serengeti boys kwani imechabangwa goli 1-0,ambapo cameroon wameambua kurudisha kipigo hicho kama walivyokubali kupokea wao kwenye mchezo wao wa awali.
Mchezo ambao umekuwa mgumu kwa upande wa serengeti boys kwani imechabangwa goli 1-0,ambapo cameroon wameambua kurudisha kipigo hicho kama walivyokubali kupokea wao kwenye mchezo wao wa awali.
Timu ya vijana ya cameroon ilipata
goli lake kwa kupitia mchezaji wake John Innocent mnamo dakika ya
(74') ya mchezo hivyo kuwafanya camerooni kumaliza mchezo wakiwa
kifua mbele kwa goli hilo hilo moja kwa bila(1-0).
Aidha mchezo ulionekana kuwa mzuri
na kila timu kutawala vizuri dimba,lakini wao cameroon wamebahatika
kutumia vizuri nafasi waliyoipata.na huu ndio ulikuwa mchezo wa
mwisho wa kujipima kwa serengeti boys kabla ya kwenda kwenye michuano
itakayofanyika Gabon.
No comments:
Post a Comment