Naibu Wazara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto, Dr Hamisi
Kigwangala amesema
kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini sasa imeimarika na kufikia
asilimia 83 ambapo
ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi wake.
Ameongeza kuwa kwa
Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe
Magufuli,upatikanaji wa dawa ni kipaumbele na kuimarisha idara ya
afya kwa ujumla,kwa kuboresha huduma kwenye vituo vya kutolea huduma
za Afya kwa umma kote nchini.
“Katika
kuhakikisha haya yamawezekan serikali ya Awamu ya Tano ilichukua
jitihada za haraka na za lazima kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka
shilingi Bilioni 31 kufikia shilingi Bilioni 251.5.ambapo ongezeko
hilola fedha hizo zimeimarisha hali ya upatikanaji wa dawa
nchini,jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari
ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma
kupata mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba pia.alimalizia” .Dr
Kigwangala
SapulaMedia android app sasa inapatikana playstore: Kwa kupata Habari za karibu kuhusu:\\ Habari, Muziki na burudani,Michezo,Technolojia,Ujasiriamali ili kupakua bonyeza link --->>>
No comments:
Post a Comment