Klabu ya Ajax ya Uholanzi
imefanikiwa kuifunga Lyon ya Ufaransa bao 4-1 katika mchezo wa nusu
fainali ya kwanza ya michuano ya Uefa Europa mchezo uliofanyika pale
uwanja Amsterdam Arena.ambapo magoli ya Ajax yamefungwa na wachezaji
Bertrand Traore mabao mawili, Kasper Dolberg, Amin Younes na huku
wapinzani wakipata goli lao toka kwa Mathieu Valbuena.
Klabu ya Juventus toka Italia
ilikuwa ugenini dhidi ya FC Monaco katika mchezo huo wa nusu fainali
ya michuano ya Klabu bingwa ulaya na wamefanikiwa kupata ushindi wa
mabao 2-0 .Mabao ya Juventus yalifungwa na Mchezaji Gonzalo Higuain
katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza na bao la pili Dakika ya 59
kipindi cha pili, na timu hizo zitarudiana tena mei 9 mwaka huu.
Manchester United wanatarajiwa
kushuka dimbani leo dhidi ya Celta vigo ambao wao watakuwa uwanja wa
nyumbani ,huku kukiwa na taarifa kuwa wachezaji wao kadhaa
watarejea dimbani baada ya kukumbwa na majeraha. Akiwemo mchezaji wao
ghali Paul Pogba.
No comments:
Post a Comment