Arsenal wameshindwa kutamba katika
uwanja wa Anfield hii leo,kwa washika mitutu hao wa London
kuendeleza rekodi mbovu ndani ya Anfield baada ya kupataa kipigo cha
bao 4-0.
Roberto Firminho alifungua dirisha
la magoli hayo dakika ya 17 kabla ya Sadio Mane kufunga dakika ya 40
na kuwa mchezaji wa pili kuifungia Liverpool mabao katika mfululizo
wa mechi tatu za mwanzo wa msimu, mabao hayo yalikifanya kipindi cha
kwanza Liverpool kwenda mapumziko wakiongoza kwa mabao mawili.
Kipindi cha pili Mohamed Salah
ambaye ndio mchezaji bora wa mchezo huu alifunga goli la tatu dakika
ya 57 kabla ya Daniel Sturidge dakika ya 77 likiwa ni goli lake la 99
kwa Liverpool na kuufanya mchezo uishe kwa matokeo ya 4 - 0.
No comments:
Post a Comment