Lile pambana la ndondi lililokuwa
likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa ndono duniani kote kati ya
bondia Floyd Mayweather na bingwa wa UFC Conor McGregor limechezwa
mapema asubuhi ya leo.
Ambapo McGregor alifanikiwa kwenda
hadi katika raundi ya 9 lakini ilipofika raundi ya 10 mambo
yalibadilika baada ya Mayweather kumshambulia sana hadi Gregor
aliyekuwa hoi sana huku ikiwa imebaki dakika 1:55 kwa pambano kuisha.
Katika raundi ya 1 na ya 2 hadi 3
McGregor alionekana alionekana kummudu Mayweather huku refa akamuonya
kutokana na aina ya upigaji wake ambapo alionekana kumpiga Mayweather
chini ya kichwa.Baada ya raundi ya 4 kuisha na Gregor kuonekana
mchangamfu, kibao kilianza kubadilika raundi ya 5 ambapo alianza
kuonekana kuchoka na ilipofila ya 8 McGregor alionekana hoi zaidi
ndipo ya 10 alishambuliwa sana akiwa hoi bina taabani.
Ushindi wa asubuhi ya leo umezidi
kumpa rekodi nzuri Mayweather ambapo sasa Mmarekani huyo anakuwa
amecheza mapambano 50 ya mashindano bila kupigwa.Baada ya mchezo huo
Floyd alisema “nimewapa mashabiki kile walichotaka kukiona, baada
ya mpambano ya Pacquao niliwaahidi kwamba nitarudi kuwafurahisha na
leo wameona nilichofanya” alisema Mayweather huku akisisitiza “ni
mpambano wangu wa mwisho”.Pambano hili lilihudhuriwa na mastaa kibao akiwemo Mike Tayson ambaye nae alitingisha kunako anga za masumbwi kidunia.
No comments:
Post a Comment