Klabu ya Manchester United
imechomoza na ushindi mnono wa magoli 4-0 dhidi ya Swansea mchezo wa
ligi kuu nchini Uingereza .Manchester United wameendeleza dozi leo
tena wakiwa ugenini kutoa kipigo kikali kwa Swansea Fc na kuendelea
kujikita kileleni mwa ligi.
Magoli ya United yakifungwa na E
Bailly dakika ya 45 wakati magoli mengine matatu yakitiwa wavuni na
Romelu Lukaku dakika ya 80, Paul Pogba dakika ya 82 huku, Anthony
Martial akihitimisha karamu ya magoli dakika ya 84 ya mchezo
huo.Vijana hao wa Jose Mourinho wameonekana kuwafiti zaidi katika
kipindi cha pili cha mchezo huo. Na imepelekea mchezo kumalizika kwa
ushindi huo mnono.
No comments:
Post a Comment