Idadi ya watu waliouwa kwnye maporomoko ya ardhi nchini Sierra
Leone bado haijulikani,ambapo eneo moja la milima liliporomoka mapema
leo Jumatatu kufuatia mvua kubwa, na kusababisha nyumba nyingi
kufukiwa na hata baadhi ya usafiri binafsi kuharibiwa vibaya kutokana
na adha hiyo.
"Tulikuwa ndani, tukasikia udongo ukikaribia, tukaanza
kutangatanga kwa kukimbia, nilijaribu kumchukua mtoto wangu, lakini
udongo ulikuja kwa haraka sana na sikufanikiwa kumuokoa”.hii ni hali
iliyowakumba raia wa eneo hilo ambapo kila mmoja alikuwa na kilio
chake kwa kulilia wapendwa aliowapoteza kwenye maafa hayo.
Maafisa wa usalama wanasema kuwa ni mapema sana kutoa idadi kamili
ya watu waliouawa,kwa mda mchache sana watu wameweza kupashana habari
hii yenye simanzi kwa kupitia mitandao ya kijamii,kwa kutumiana picha
za mafuriko kwenye eneo la ndani na nje ya mji wa Free town.
No comments:
Post a Comment