Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Misri
Abdel Fattah Al Sisi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.
Aidha Rais Magufuli aliongozana na
viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Makamu wa Rais, Bi Samia
Hassan Suluhu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais wa Zanzibar,amabpo
Rais huyo yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi
alikagua gwaride la Heshima mara baada ya nyimbo za Taifa kupigwa
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) jijini
Dar es Salaam,Pia mgeni huyo alipata fursa ya kuangalia vikundi vya
ngoma za asili mara baada ya kuwasili nchini.
No comments:
Post a Comment