Baadhi ya raia wa kenya wameonekana
kupuuza wito kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga wa kususia kazi
leo kwa kusisitiza kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi wa
urais,ambapo siku kadhaa zilizopita biashara nyingi zilifungwa huku
watu wakihofia kuzuka kwa fujo kutokana na hali ya siasa baada ya
uchaguzi.
Tofauti na hapo awali kwani kwa
sasa, biashara zimeanza kufunguliwa,baadhi ya wanachi wa kenya
wakionekana kwenye maeneo tofauti wakiendelea kufanya kazi kujipatia
riziki zao.
Rais Kenyatta alipata kura 8, 203,
290 ambayo ni asilimia 54.27 naye Bw Odinga akapata kura milioni
6,762,224 ambayo ni asilimia 44.74.
Bw Odinga, aliyewania urais kupitia
muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa) amekataa kukubali
matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(IEBC). Nao Muungano wa Nasa umedai mitambo ya tume ya uchaguzi
ilidukuliwa na matokeo kuchakachuliwa kuhakikisha Bw Kenyatta
anashinda.
Waangalizi wa kimataifa kutoka
Umoja wa Afrika, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola, miongoni mwa
wengine, ambao walisema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
No comments:
Post a Comment