Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameongea na wasamii wa Filamu na
kuwaeleza mikakati ya Serikali katika kutatua changamoto za tasnia
yao kote nchini kwenye kikao maalumu kilichowakutanisha leo jijini
Dar es Salaam.
Walijitokeza wasanii lukuki katika kupata kile
walichotakiwa kukijadili kwa maslahi ya wasanii na tasnia nzima ya
filamu hapa nchini,na baada ya mazungumzo na majadiliano hayo Waziri
Harrison aliamaliza kwa picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa
filamu.
No comments:
Post a Comment