Rais Magufuli leo ameanza ziara ya
kikazi ya siku tano mkoani Tanga,akiwa huko amesema Serikali imeanza
kuchukua hatua dhidi ya watu waliouziwa mashamba makubwa Mkoani Tanga
na kuyatelekeza ambapo mpaka sasa hati miliki 5 za ardhi zenye zaidi
ya ekari 14,000 zimefutwa na utaratibu unaendelea ili kuwagawia
wananchi na wawekezaji watakaokuwa tayari kuyaendeleza kama
ilivyokusudiwa.
Pia Rais Magufuli ameagiza shamba
la ekari 50 lililopo katika kijiji cha Kabuku ambalo lililotolewa na
wananchi kwa Jeshi la Kujenga Taifa “JKT” kwa lengo la kujenga
kiwanda miaka 7 iliyopita, lirudishwe kwa wananchi na ameitaka “JKT”
ijenge kiwanda hicho katika eneo lake jingine lenye ukubwa wa zaidi
ya ekari 9,000.
Aidha, Rais Magufuli ametoa siku 15
kufanyika kwa uchunguzi wa fedha Tsh. Milioni 500 zilizotolewa kwa
ajili ya ujenzi wa majengo ya kituo cha afya cha Mkata, kufuatia
kuwepo kwa taarifa za ufujaji wa fedha hizo na kuongeza kuwa Serikali
itapeleka Tsh. Milioni 800 kwa ajili ya kuendeleza kituo hicho baada
ya hatua stahiki kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment