Singida United imesaini mkataba wa
mwaka mmoja na kampuni ya utengenezaji wa mbolea ya YARA Tanzania
kutoka Norway.Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi wa Singida United
Festo Sanga na Mkurugenzi wa kampuni ya YARA Alexander Macedo.
Mkurugenzi wa kampuni ya YARA,
Alexander Macedo amesema wameamua kuidhamini klabu hiyo kwakua
anapenda mpira na kilimo na anaamini kupitia wao vijana wengi wa
Tanzania watapata ajira.
Mkuugenzi wa Singida United Festo
Sanga amesema wanaendelea kutafuta wadhamini wengine ambapo kwa sasa
wapo kwenye mazungumzo na makampuni mengine zaidi.Aidha mbali na
kampuni hiyo tayari timu hiyo imeingia mkataba na ya SportPesa, Oryx
na Puma kama wadhamini rasmi wa klabu.
No comments:
Post a Comment