Mmoja wa viongozi wakuu wa kanisa
la kianglikana nchini Uganda, amesema kuwa hatahudhuria mkutano
unaokuja wa viongozi wa kanisa la Anglikana ambao utafanyika mwezi
Oktoba nchini Uingereza, kwa sababu hakubaliani na wale ambao
wameanza kukubali ndoa za jinsia moja.
Askofu mkuu wa Uganda Stanley
Ntagali ameeleza kuwa hayupo tayari kukutana na wale wanaokubaliana
na ndoa zinazoenda kinyume na na mafunzo ya Biblia na ametanabaisha
kuwauamuzi wake umekuja baada ya kuomba ushauri kutoka kwa viongozi
wengine nchini Uganda.
Wakatai wa mkutano uliopita wa
viongozi wa dunia uliofanyika Januari mwaka 2016, Askofu Stanley
Ntagali aliamua kuondoka mapema na kusema hatorudi tena ikiwa hali
hiyo haitarekebishwa.
No comments:
Post a Comment