Mwanariadha wa Afrika Kusini Wayde
van Niekerk, anatarajiwa kuchukua kijiti katika kuwa kinara kama
mwanariadha bingwa duniani baada ya bingwa Usain Bolt kustaafu.
Bolt atastaafu katika riadha baada
ya mashindano ya riadha ya ubingwa wa dunia ambayo yataanza jijini
London siku ya Ijumaa.Bolt amekuwa kivutio kikubwa cha riadha baada
ya kushinda mbio za mita 100 na 200 mjini Beijing mwaka 2008.
"Van Nieker ameonyesha kuwa
yeye ni nyota wa dunia." ameeleza Usain Bolt ,Van Niekerk
alishinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 400 katika
mashindano ya mwaka uliopita ya olimpiki ya Rio kwa muda wa sekunde
43.03.
No comments:
Post a Comment