Mshambuliaji wa Brazil Neymar
amesema kuwa alihitaji changamoto mpya , wakati anapojiunga na klabu
ya PSG kutoka Barcelona kwa kitita kilichovunja rekodi ya uhamisho
cha (£200m).Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alishinda mataji
saba muhimu katika misimu yake minne katika uwanja wa Nou Camp
ikiwemo taji la klabu bingwa mara moja na lile la La Liga mara
mbili.Neymar amesema kuwa baba yake alimtaka kubaki Barcelona
Ameandika kwenye Instagram akaunti
yake: Nimeshinda mataji yote ambayo mchezaji soka anafaa
kupata.”Nimeishi maisha ambayo siwezi kusahau, lakini mchezaji
anahitaji changamoto'',''Na kwa mara ya pili katika maisha yangu,
ninakwenda kinyume na matakwa ya baba yangu''.
Uhamisho wa Neymar umevunja rekodi
ya awali iliyowekwa na Paul Pogba aliporudi kuichezea Manchester
United kutoka Juventus kwa kitita cha £89m mnamo mwezi Agosti
2016.Huku mshahara wake ukiwa £782,000 kwa wiki.Neymar anatarajiwa
kutambulishwa mbele ya mashabiki wa PSG kwenye uwanja wa Parc des
Princes siku ya Jumamosi.
No comments:
Post a Comment