Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake, Rais wa
Uganda Yoweri Museveni wakivuta utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la
msingi la mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda
hadi Tanga huku viongozi mbalimbali wa Tanzania na Uganda
wakishuhudia. Shughuli hiyo ilifanyika katika kijiji cha Chongoleani
nje kidogo ya jiji la Tanga.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Uganda
Yoweri Museveni wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari
mbalimbali waliohudhuria shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi la
mradi mkubwa wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Tanga.
Na baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais Magufuli,mke wake Mama
Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa waliweza kumuaga Rais wa Uganda Yoweri Museveni
kwenye uwanja wa ndege wa Tanga.
Wananchi
waliojitokeza kwa wingi kushuhudia zoezi hilo walionekana wakifurahia
wakati wa hotuba ya Rais Magufuli na hivyo kulifanya zoezi hilo
kukamilika katika hali ya kufana,lakini pia wasanii waliweza
kutumbuiza na kuonesha hali ya uzalendo na nyuso zao za bashasha.
No comments:
Post a Comment