Tume ya
Uchaguzi nchini Rwanda , imemtangaza Rais Paul Kagame kuwa mshindi wa
kiti cha Uraisi katika uchaguzi uliofanyika jana.Rais Kagame ambaye
amekuwa madarakani kwa miaka kumi na saba, ameshinda nafasi ya Uraisi
kwa kupata asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa baada ya uchaguzi huo.
Uchaguzi huyo ulihusisha chama cha
Rais Paul Kagame (Rwandan Patriotic Front )RPF, chama Green Party cha
Frank Habineza na Philippe Mpayimana, mgombea huru.
Baada ya matokeo hayo wapinzani wa
Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao walisumbuliwa wakati wa kampeni
hali iliyopelekea kutokuwepo kwa wapiga kura wa kutosha jambo ambalo
limepingwa na chama tawala.
No comments:
Post a Comment