Kocha wa Singida United Hans van
Pluijm ameonekana kuridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji
wake kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga licha ya kufungwa 3-2
na mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania bara.
Pluijm amesema wachezaji wake
wamecheza kwa kwa kufuata maelekezo japokuwa kulikuwa na makosa
machache ambayo benchi la ufundi watakaa na kuyafanyia kazi.
“Wamecheza
kwa kuzingatia maelekezo tuliyowapa licha ya kupoteza mechi lakini
bado nimevutiwa sana kiufundi na hicho ndio kitu muhimu tulichokuwa
tunakitaka.”
Magoli ya Yanga yamefungwa na
Thabani Kamusoko, Amisi Tambwe na Emanuel Martin wakati Singida
United wao walifunga kupitia kwa Danny Usengimana na Shafiq
Batambuze.
No comments:
Post a Comment