Klabu ya
Arsenal imefanikiwa kuchukua Kombe la ngao ya jamii 2017 kwa kuifunga
Chelsea goli 4-1 kwenye mikwaju ya penati baada ya kutoka sare ya 1-1
kwenye dakika 90, katika uwanja wa taifa wa Uingereza, Wembley.
Chelsea walianza vizuri kipindi cha
kwanza kwa kukosa magoli mengi lakini kipindi cha pili kunako dakika
ya 47 walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Victor Moses.Chelsea
waliendelea kumiliki mpira mpaka dakika ya 81 baada ya Pedro
Rodriguez kupata kadi nyekundu na kutolewa uwanjani kwa kumchezea
rafu Sead Kolašinac.
Kadi hiyo nyekundu ilibadili upepo
kabisa kwani dakika moja mbele 82 Arsenal walisawazisha kupitia kwa
Sead Kolašinac, mpaka kipenga cha mwisho matokeo.Kwa matokeo timu
zote mbili ziliingia kwenye hatua ya mikwaju ya penati ambapo
Chelsea walipigwa magoli 4-1.
No comments:
Post a Comment