Usain Bolt ameshindwa kustaafu
riadha akiwa kinara baada ya kushindwa wakati wa mbio za mita 100
kwenye mashindano ya IAAF mjini London.Bolt alimaliza mbio hizo
katika nafasi ya tatu na kushinda shaba huku Christian Coleman mwenye
umri wa miaka 21 akichukua nafasi ya pili.
Licha ya
Gatlin kuibuka bingwa wa mita 100 mwaka 2004 na bingwa mara mbili
mwaka 2005, alionekana kutokubalika kwa mshabiki kutokana historia
yake ya kupigwa marufu kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za
mwili,hata hivyo mwaka 2006 aliponea chupu chupu kufungiwa maisha
kushiriki mchezo huo mpaka pale alipokubali kushirikiana na mamlaka
na kukubali marufuku ya miaka nane ambayo baadaye ilipunguzwa hadi
miaka minne baada ya kukata rufaa.
Hatua hiyo ilimruhusu kurejea tena
mbioni,hata hivyo mashabiki walio wengi walionekana wakimshangilia
Usain Bolt wakati matokeo yakitangazwa na hata kwenye wakati mchezo
ukiendelea,hii ni mara ya kwanza kwa Bolt kushikilia nafasi hiyo
kwenye mbio za mita 100 katika ubingwa wa dunia.
No comments:
Post a Comment