Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa
wapiga kura nchini humo kuondoka kwenye vituo vya kupigia kura na
kwenda nyumbani baada ya kupiga kura.hayoameyaongea katika hotuba kwa
taifa kabla ya uchaguzi mkuu Jumanne, amesema wananchi wapige kura
kwa amani.
Awali muungano wa upinzani
uliwashauri wafuasi wake kutoondoka vituo baada ya kupiga kura “
ili kulinda kura”,Lakini baadaye, muungano huo ulibadilisha mtazamo
huo na kuwashauri waondoke baada ya kupiga kura.
"Bila kujali matokeo ya
uchaguzi huu, ni lazima tuendelee kushikamana kwa pamoja kama
wananchi. Na kikubwa zaidi,tukatae ghasia au majaribio yoyote ya
kutugawa," aliongeza Kenyatta.
No comments:
Post a Comment