Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaonya watanzania wenye tabia ya
uvivu kuwa katika utawala wake hata toa vitu vya bure kwa watu ambao
hawataki kujituma kwenye kazi wakisubiri msaada.
Akihutubia wananchi wa wilaya ya
Korogwe mkoani Tanga waliohudhuria uzinduzi wa kituo cha mabasi
(Stand) wilayani humo, Rais Magufulina amesema kuwa watu wanaopenda
kukaa vijiweni bila kujishugulisha huku wakilalamika njaa na hakuna
pesa, ni bora wafe na njaa.
“Wakati wa kukaa kwenye magenge
na kupiga maneno umepitwa na wakati, mnakaa kwenye pool unasubiri
vitakuja hakuna, vya namna hiyo nataka kuwaeleza havitakuja kwenye
utawala wangu, mnakaa mnasubiri tuna njaa tunataka mtuletee, mimi
njaa nafuu ikuue kuliko nikuletee chakula, kwa sababu kama mwenzako
ana chakula wewe una njaa, hatuwezi tukavumilia vitu vya namna hiyo”,
amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli
amesisitiza kuwa dhamira yake ni kuifanya Tanzania iendelee kwa
kusonga mbele kwahiyo hataogopa chochote ataendelea kuongea ukweli
hata kama wavivu watamchukia.
No comments:
Post a Comment