Zaidi ya watu 400 wamekamatwa
katika oparesheni dhidi ya ugaidi nchini Malaysia,na waliokamatwa
kwenye mji mkuu Kuala Lumpur walikuwa ni kutoka nchini Bangladesh,
India na Pakistan.
Vimenaswa vifaa vya kutengeneza
passport bandia na na baadhi ya stakabadhi zisizo halali za uhamiaji
za Malaysia.Mamlaka zinasema kuwa zinalenga yeyote asiye na stakadhi
za usafiri na yeyote ambaye anaaminika kuwa na uhusiano na makundi ya
kigaidi nchini Syria na Iraq.
"Tutawatambua na kuwachukulia
hatua wageni wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na magaidi, hasa
wanaohusika na mambo tofauti nchini Syria," aliongeza afisa wa
kupambana na ugaidi Ayob Khan Pitchay.
No comments:
Post a Comment