Spika Mstaafu Anna Makinda
ameipongeza DCB Commercial Bank kwa huduma bora za kibenki amewaasa
DCB Commercial Bank kujikita zaidi kutoa huduma hii kwa
wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambao ndiyo wengi nchini ili
kuboresha hali za maisha yao kwa kuwapatia mikopo.
Hayo
aliyasema wakati alipotembelea banda la DCB Commercial bank katika
maonesho ya nane nane kanda ya kati yanayoendelea mkoani Dodoma.
Makinda aliongezea kuwa ili kuwezesha wajasiriamali wengi DCB Benki
haina budi kupeleka huduma hii ya mikopo nafuu kwa wajasiriamali
wadogo wadogo vijijini ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii ya
mikopo ya vikundi Sambamba na utoaji wa mikopo hii ya vikundi kwa
wajasiriamali wadogo wadogo.
Makinda ameasa DCB kuwaunganisha
wajasiriamali hawa na huduma ya bima ya afya kutoka NHIF na pia bima
ya taifa ya Jamii ili wateja hawa au familia zao wanapougua wapate
msaada wa matibabu kwa unafuu hivyo kuwafanya wawe na afya na kuweza
kurejesha mikopo .
Spika Mstaafu Anna Makinda akikaribishwa na
Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame katika
banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa
Dodoma.
No comments:
Post a Comment