Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amekabidhi hatimiliki 88 kwa
wakazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam ambapo hati 4333 ambazo ziko
kwenye hatua za mwisho katika mradi wa urasimishaji wa makazi holela.
Mhe. Lukuvi amesema hizi hati ni
mtaji uliofufuliwa baada ya wakazi kukaa na kuendeleza maeneo
yasiyopimwa ,hivyo kuondokana na mtaji mfu kwani hakuna mtu yeyote
ambaye angeweza kupata mkopo bila ya kuwa na hati.
Mhe. Lukuvi amesema kuwa Serikali
ya awamu ya Tano inayo dhamira ya dhati ya kurasimisha makazi nchi
nzima ili kuongeza thamani ya ardhi au maeneo husika. Ardhi yenye
hatimiliki thamani yake inaongezeka kwani inatambuliwa na taasisi za
fedha ambazo ni rahisi kukopesha wenye hati.
“Kwa hati hizi zilizotolewa
takribani 4333 tukisema kila nyumba ikopeshwe kwa kiwango cha chini
cha shilingi milioni 10, kwa siku ya leo Kimara inapata mtaji wa
karibu bilioni 40.5”.aliongeza Waziri Lukuvi.
No comments:
Post a Comment